
Faida ya Kutangaza Baisahara yako Kwenye Mitandao ya Kijamii ( Instagram, Facebook, Twitter)
Mitandao ya Kijamii imeweza kukutanisha watumiaji wengi ulimwenguni. Ikiwemo akaunti za watu binafsi na za biashara. Biashara kwenye mitandao ya kijamii zimekuwa zikiongezeka siku hadi siku, watumiaji pia wa mitandao hii wamekuwa wakiongezeka siku hadi siku. Hivi sasa mitandao ya kijamii inawatumiaji zaidi ya Billion Moja duniani kote. Hapa Tanzania watumiaji wa mitandao ya kijamii wana kadiriwa kuwa 5.4million, hii ni asilimia 8.9% ya idadi yote ya wananchi wa Tanzania.
Kwa idadi hii kubwa ya watumiaji, kunawapa wafanyabiashara wigo mkubwa zaidi ya kutangaza, kuanika biashara zao kwa watu wengi zaidi
kwa kutumia mitandao hii ya kijamii. Lakini swali la kujiuliza unafanyaje ukiwa unafollowers wachache, na unafahamu mtandao huo wa kijamii unawatu zaidi ya million kadhaa ambao pia wangeweza kuwa wateja wa biashara yako?? Ili kufikia hawa watumiaji wengine ambao sio followers wako au marafiki zako kwenye mtandao huo wa kijamii kama vile instagram, facebook, twitter na kadhalika unabidi utumie mfumo wa matangazo ndani ya mitandao hii unaoitwa “Sponsored Ads” .
Kabla hatujapata ufafanuzi zaidi wa “Sponsored Ads” Ngoja tuangalie takwimu ya mtandao wa Facebook, Instagram na Linkedin. Mtandao wa kijamii wa Facebook unakadiliwa kuwa na watumiaji zaidi ya Million 4 nchini Tanzania asilimia 64% ya hawa ni wanaume, na asilimia 37.5% ifuatayo wanakadiriwa kuwa wanawake.
Mtandao wa kijamii wa Instagram, unakdiliwa kuwa na watumiaji zaidi ya Million 2.8 nchini Tanzania. Kati ya hawa Asilimia 58.6% ni wanaume na asilimia 41.4% ni wanawake.
Sponsored Ads:
Sponsored Ads ni mfumo wa matangazo kwenye mitandao ya kijamii unaowawezesha mtumiaji wa mtandao huo wa kijamii kufikia hata watu ambao hafahamiani nao au sio followers wao. Mfumo huu wa matangazo unatozwa kwa idadi ya watu waliona tangazo au idadi ya watu walio bofya kwenye tangazo hilo. Mfumo huu unawezesha biashara au mtu bianfsi kufikia maelfu ya watumiaji wa mtandao huo wa kijamii na kuwezesha kuuza, kutangaza biashara zao, au kuongeza followers wao kwa kulipia gharama ya mfumo huo wa matangazo.
Tofauti ya Sponsored Ads na kutangaza kwenye account ya mtu mwenye followers wengi na hapa hatu maanishi mtu maarufu au kwa jina lingine (influencer). Ni kuwa kupitia mfumo wa sponsored ads mtangazaji wa mtandao wa kijamii anauwezo wa kuchagua ni watu gani walengwa haswa watangazo hilo, kwa kutumia vichujio kama miaka yao, jinsia yao, mahali walipo, wanachopenda kufanya (interests zao) nakadlika. Vichujio hivi vinamsaidia mtangazaji kupata au kulenga wateja haswa watakaoweza kununua bidhaa au kutumia huduma yake. Hii ni tofauti na kutangaza tuu biashara yako kwenye account ya mtu mwenye followers wengi, ambao hauna huwakika ni followers wa umri gani, wanapenda nini, kama watapenda bidhaa yako au kama wanauhitaji wa bidhaa yako au la. Hii kutokufahamu yote inauwezo wakuto kuletea matokeo mazuri kwenye tangazo lako mfano watu wanaweza kuliona lakini kusiwepo hata mmoja wa kununua bidhaa au huduma yako, matokeo yake ni upotevu wa muda, mapato na nguvu.
Faida nyingine ya kutumia sponsored ads na sio kutangaza kwenye page ya mtu mwenye followers wengi ni uwezo wa kuona namna tangazo lako linavyofanya kazi na kuona takwimu kama idadi ya watu walioliona, watu wangapi walibofya kwenye tangazo lako, umri wao na kadhalika.
Gharama za kutangaza:
Pata views kati ya 3500 mpaka 7000 pamoja na likes kwenye tangazo lako, na ukuze biashara yako leo. Kwa bei ya 35,000Tshs tuu tunakutangazia tangazo lako wiki nzima, na tunakupa offer ya kutengenezea tangazo (Poster) lako kwa ufanisi Buree. Wahi sasa.
Tunahudumia makampuni na taasisi tofauti tofauti kama vile makampuni binafsi, ya serikali, maduka, wapambaji, biashara za bakery, maduka ya nguo, maduka ya viatu, maduka ya urembo, maduka ya electronics, real estate, madalali wa nyumba nakadhalika. Kwa wateja wenye mahitaji zaidi ya kutangazia kwenye mitandao ya kijamii ( Instagram na Facebook) na unahitaji huduma zingine kama social media account management, search engine optimization services, social media marketing management, website design and development tumbelea page yetu ya Service kwa maelezo zaidi na gharama zake.
Hivyo kama kampuni (InnoveMarketing) iliyobobea kwenye matangazo ya mitandao ya kijamii, tunashauri mfanyabiashara kutumia mfumo wa Sponsored Ads, ili kuweza kufikia walengwa kwa urahisi, na kuongeza mauzo ya biashara yako. Kwa msaada wa kutengenezewa tangazo litakaloweza kuongezea mauzo ya biashara yako na kuwafikia wateja wengi zaidi mtandaoni, wasiliana nasi sasa ilituweze kukusaidia.